Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto katika hafla ya awali. [Picha/ abc.net.au]
Baraza la wazee wa jamii ya Mijikenda Kaunti ya Mombasa limetangaza kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta kwenye marudio ya uchaguzi wa uraisi wa Oktoba 26.
Akiwahutubia wanahabari siku ya Jumatatu, mwenyekiti wa baraza hilo Stephen Ruwa alisema kuwa serikali ya Jubilee imewaletea wakaazi wa Mombasa maendeleo mengi, kinyume na madai ya upinzani.“Jubilee imewaletea Wapwani maendeleo mengi hasa katika Kaunti ya Mombasa, kinyume na vile upinzani unavyotuambia,” alisema Ruwa.Ruwa alisema kuwa baraza hilo litahakikisha kuwa Jubilee inajinyakulia kura nyingi jijini Mombasa.“Tutahakikisha wamijikenda wote wanampigia kura Rais Kenyatta ili aweze kutuletea maendeleo Zaidi,” alisema Ruwa.Ruwa amewaomba Wapwani kuchagua viongozi wenye malengo ya maendeleo na kupuuza siasa za mrengo wa NASA.Raisi Uhuru Kenyatta katika hafla ya awali, .Awali.Wazee wa kimijikenda watangaza kuunga mkono Jubilee kwenye marudia ya uraisi.