Gavana wa Kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua ameahidi kukarabati makao ya wazee yaliyo katika mtaa wa Kivumbini kwa kima cha shilingi milioni tisa.
Gavana Mbugua amesema kuwa serikali yake imetenga pesa hizo ambazo zitafanya upanuzi wa makao hayo, sawa na kukarabati kituo hicho kwa ujumla ili kiweze kusitiri wazee zaidi.
Aidha amewataka wakaazi wa kaunti ya Nakuru na wananchi kwa jumla kuweka kando dhana ya kwamba wale wanaoishi katika makao ya wazee ni watu maskini.
kadhalika ameongeza kuwa licha ya kuboresha makaazi hayo serikali yake itahakikisha kwamba afya ya wazee hao inazingatiwa kikamilifu kwa kupewa dawa na matibabu mengine.
vilevile amesisitiza kuwa atahakikisha kuwa lishe ya wazee hao inazingatiwa ipaswavyo ikiwa ni kwa mujibu wa sera za kaunti sawa na sera za serikali ya Jubilee ya kuwajali wazee.