Kaunti ya Kisii imeombwa kuingilia kati kusaidia watu walioadhiliwa na funza katika kaunti hiyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hii ni baada ya Kaunti hiyo kuwa miongoni mwa kaunti zilizo adhiliwa sana na janga la funza.

Akiongea Jumatatu katika kijiji cha Nyangiti, Joash Mogusu, alisema kuwa kuna haja ya serikali ya kaunti kuwasaidia watu ambao wamevamiwa na funza.

Baadhi ya watu wengi waliovamiwa na funza ni wazee ambao ni wajane na wengine wanaishi kwa umaskini.

Chifu wa eneo hilo John Ogega aliwaomba wanakijiji kusaidia wasiojiweza.

“Tunapswa kuwa majirani wema. Tusaidie wenzetu walioko na shida ili waweze kuishi vyema,” akasema Ogega.

Mary Wamboi, kutoka Ahadi Kenya, na mmoja wa walioongoza shughuli hiyo alisema kuwa wametembelea maeneo ya Kisii na ile ya Nyamira baada ya kugudua kuwa baadhi ya wakaazi wamelemewa na shida ya funza.

Kepha Ombasa ambaye ni mhudumu wa kijamii analaumu serikali ya kaunti kwa kukosa kushughulikia swala la funza vilivyo.

“Kama makundi ya kijamii tumejaribu kupigana na tatizo hili lakini hatujapata msaada wa kutosha kutoka kwa serikali ya kaunti,” akasema Ombasa.

Alisema kuwa waziri wa afya katika kaunti hiyo halichukuia swala la funza kwa uzito.

“Waziri hutuambia tuwashauri walio na chawa waoge ili shida hii iwaodokee,” akasema Ombasa.

“Kwa sasa ni wahisani wema na viongozi ambao wana moyo wa kupambana na janga hili ambao wanasaidia; sisi hupata dawa za kuwashughulikia walio vamiwa na funza kutoka kwa makundi yasiyo ya serikali,” akasema Ombasa.