Waziri wa viwanda Aden Mohammed.[kenyanewsagency.go.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Waziri wa viwanda Aden Mohammed amesema gharama za umeme ndio sababu kuu ya serikali kufanikisha kuhamisha utendakazi wa bandari ya Mombasa hadi katika kaunti ya Naivasha.

Waziri Mohammed ameelezea kuwa Naivasha ina uwezo wa kuzalisha umeme ulio rahisi na wenye kuaminika.

Akizungumza katika warsha ya wanachama wa kamati ya kitaifa ya biashara,viwanda na vyama vya ushirika jijini Mombasa siku ya Jumapili, waziri huyo alisema kuwa hatua hiyo itaweza kubuni nafasi zaidi ya ajira kwa vijana wa kaunti ya Mombasa pamoja na ile ya Naivasha kinyume na inavyodhaniwa na baadhi ya wanasiasa wa Mombasa.

Amewataka viongozi wa Mombasa kutoigiza siasa katika swala zima la uhamisho wa bandari hiyo.

Ikumbukwe gavana wa Mombasa Hassan Joho na baadhi ya viongozi wa Mombasa wamekuwa msatari wa mbele kupinga kuhamishwa kwa utendakazi wa bandari hiyo,wakisema kuwa hiyo ni njama ya kuwapokonya wapwani raslimani yao kuu.

Wakati huo huo waziri Mohammed aliwaomba wanachama wa kamati hiyo kushirikiana na kuweza kupitisha miswaada ambayo itaweza kufanikisha miradi tofauti kote nchini ili kukuza uchumi wa taifa.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Kanini Kega alisema watatengeza sheria mwafaka ili kuhakikisha kwamba shugli za wizara hiyo zimefaulu.