Waziri wa Elimu Dkt Fred Matiang’i anatarajiwa kuongoza hafla ya tatu ya sherehe za mahafali ya Taasisi ya Mafunzo ya Teknologia ya RIAT (Ramogi Institute of Advanced Technology), Kaunti ya Kisumu, mnamo Machi 24.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza kwenye mahojiano na mwandishi huyu afisini mwake siku ya Jumanne, Mwalimu mkuu wa Taasisi hiyo Bwana Jorim Guya, alisema kuwa wamewasiliana na waziri huyo kupitia barua na simu, na ameahidi kuongoza sherehe hizo.

“Maandilizi ya sherehe hizo za mahafali yanaelekea kukamilika na mgeni wa heshima atakua Waziri wa Elimu Dkt Fred Matiang’i. Vile vile, tunatarajia wageni wengine wengi,” alisema Bwana Guyo.

Guyo alisema kuwa wanafunzi zaidi ya elfu moja wanatarajiwa kufuzu, baada ya kusomea taaluma mbali mbali katika taasisi hiyo.

Licha ya taasisi hiyo kuanzishwa mwaka wa 1976, sherehe za mahafali zitaandaliwa kwa mara ya tatu katika historia ya taasisi hiyo, kutokana na kile Bwana Guyo alikitaja kama watangulizi wa chuo hicho kutotilia maanani umuhimu wa sherehe hizo.

Bwana Guyo alisema kuwa wameamua kuwa sherehe hizo za mahafali zitakua zikiandaliwa kila mwaka kwenye taasisi hiyo.