Madereva katika kituo cha magari mjini Kisii wamewakosoa wanaozoa taka katika mji huo kwa kukawia kuzoa taka hizo zinazo harufu mbaya.
Hii ni baada ya harufu mbaya kusababishwa na uchafu huo ambao umetapakaa kwenye kituo hicho cha magari ambao bado haujatolewa kwa siku kadhaa sasa.
Wakiongea na Mwandishi wa Habari huyu siku ya Jumatano mchana, wengi wa Madereva katika kituo hicho, walikashifu kitendo hicho wa kutozoa taka kutoka eneo hilo.
“Harufu ambayo hutoka kwenye uchafu huu unanuka mno, hata tumeshindwa la kufanya na tunauliza Serikali ya Kaunti ya Kisii kuwa walioajiriwa kuzoa taka kazi ya ni ipi?,” auliza Brighton Ong’era mmoja wa madereva hao.
Kulingana na sheria za mazingira nchini, uchafu haustahili kuachwa utatapakaa jinsi inavyoshuhudiwa katika kituo cha magari cha Kisii.
“Wasimamizi wa mazingira sasa wako wapi watusaidie kutatua changamoto hizi ambazo zinaendelea kutukumba na hata huenda tukapata maradhi yasioeleweka kutokana na harufu mbaya kutoka kwenye taka hizo,” alihoji Samson Osoro utingo wa gari la Kisii Classic.
Kwa upande mwingine abiria wamesema katika kituo hicho pia walilalamikia Serikali ya Kaunti hiyo kwa kuzembea katika juhudi zake za kuzoa taka katika mji huo huku wakisema hali hiyo inaweza sababisha wakaazi pamoja na wanaosafiri kupata maradhi mbali mbali.