Chama cha ODM tawi la Bungoma kimemlaumu seneta wa Bungoma Moses Wetangula kwa migawanyiko inayodaiwa kukumba muungano wa upinzani CORD.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwenyekiti wa ODM kaunti ya Bungoma John Waluke amenukuliwa kwenye vyombo vya habari akidai kuwa seneta Wetangula anatumika kama kibaraka wa Jubilee kusambaratisha mrengo wa CORD na hivyo ametaka ndoa kati ya vyama vya ODM na FORD Kenya kufika kikomo haraka iwezekanavyo.

Mbunge huyo wa Sirisia pia alipuuzilia mbali hatua ya Wetangula kuzindua azma ya kuwania urais akidai lengo lake ni kutwaa kiti cha spika au kiongozi wa wengi na sio urais.