Share news tips with us here at Hivisasa

Wanachama wa muungano wa Cord walijumuika pamoja mjini Nairobi siku ya Jumanne kushuhudia kuapishwa kwa mbunge mpya wa Malindi Willy Mtengo.

Mtengo aliyeshinda kiti hicho kupitia chama cha ODM kwenye uchaguzi mdogo aliapishwa rasmi siku ya Jumanne tayari kuanza majukumu yake kama mbunge wa Malindi.

Kinara wa Cord Raila Odinga, naibu kiongozi wa chama cha ODM ambaye pia ni Gavana wa Mombasa Hassan Joho pamoja na viongozi wengine walihudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika jengo la bunge.

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir alimpongeza Mtengo kwa hatua hiyo aliyoifikia huku akimkaribisha katika bunge.

Sasa Mtengo anatarijiwa kuchukua fursa hiyo kuwakilisha wananchi wa Malindi na kuleta mageuzi pamoja na kutimiza ahadi alizotoa wakati wa kampeni.

Mtengo alimshinda mwenzake wa Jubilee Philip Charo katika uchaguzi mdogo wa Malindi uliofanyika wiki mopja iliyopita.

Mwingine aliyehapishwa ni Seneta mpya wa Kericho Aaron Cheruiyot aliyeshinda kiti hicho kwa tiketi ya JAP.