Huenda kukatoa hali ya kutoelewana katika mrengo wa Cord baada ya vyama tanzu vya mrengo huo ambazo ni ODM na chama ya Wiper kushikilia kuwa zitakuwa na wagombea katika ntyadhfa zote za uongozi katika kaunti ya pwani.
Akiongea mjini Mombasa siku ya Jumapili Seneta wa Mombasa Hassan Omar ambaye pia ni katibu wa kudumu katika chama cha Wiper alisema kuwa chama hicho kitakuwa na wagombea katika viti vyote kuanzia ile ya gavana hadi kwa wawakilishi wa wadi.
Aidha seneta huyo alishikilia kuwa ni demokrasia ya kila mkaazi wa mombasa kumchagua mtu anayemtaka awe kiongozi na wala si kuchaguliwa na chama.
hata hivyo seneta huyo alishikilia kuwa mrengo wa Cord uko imara na wala haiwezi kusambaratika kwa sababu ya kutoelewana wa kibinafsi baina ya baadhi ya wanachama katika mrengo huo.