Wito umetolewa kwa serikali kuu hili iwafidie waathiriwa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007/2008.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya waathiwa wa kaunti hiyo ya Nyamira kuandamana hadi makao makuu ya kaunti hiyo siku ya Ijumaa walimpelekea gavana wa kaunti yao Bw John Nyagarama vilio vyao, na vile vile wakamwomba awasaidie kwa kutuma wito wao kwa serikali kuu.

"Tumeteseka sana kwa muda mrefu na tumekuwa tukiahidiwa kuwa tutafidiwa lakini wapi, tunataka gavana wetu atusaidie hili nasi tufidiwe" walisema waathiriwa hao.

Gavana aliwaambia kuwa amewasikia na akasema kuwa atatuma tetezi zao kwa serikali kuu na iwapo haitawafidia, basi serikali ya kaunti yake italishugulikia jambo hilo.