Kanisa la Got Calvary Legion Maria mjini Kisumu lilikamilisha hafla ya maombi maalumu ya toba na kufunga huku likiombea amani ya taifa na utangamano miongoni mwa jamii ya wakenya.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kwenye hafla hiyo ya maombi ambayo yalidumu kwa muda wa siku tatu mtawalia, waumini wa kanisa hilo walijumuika kwenye kanisa la Mtakatifu Michael lililoko katika eneo la Ombeyi mjini Kisumu kuanzia siku ya Alhamisi wiki iliyopita hadi Jumapili kileleni mwa maombi hayo wakati ibaada ya amani ilipoandaliwa.

Wakati wa ibaada hiyo ambayo iliongozwa na kiongozi wa kanisa hilo kanda ya Kisumu Askofu Mkuu, Isaac Benjamin hotuba maalumu ilisomwa ikituma ujumbe kwa Serikali ya kitaifa kulinda raia wake na kupigana na ufisadi kwa njia ya uwazi na usawa ili kurejesha hali halisi ya utawala huru.

“Tunatoa kauli yetu kwa Serikali Kuu ya taifa la Kenya kufanya kila iwezalo kuhakikisha amani na usalama miongoni mwa wananchi wake. Vita dhidi ya ufisadi ni lazima vipigwe kwa uazi bila mapendeleo yoyote,” alisema Askofu Benjamin.

Askofu huyo mkuu alihimiza viongozi wote wa Serikali kumrejelea Mungu ili kuliponya taifa la Kenya, akisema kuwa Mungu anapenda taifa la wenye kumtii, kumcha, kumtumainia na kumtumikia.

“Taifa lisilomcha Mungu haliwezi kusimama, na huenda likapigwa vita na Mungu Mwenyewe hadi kuporomoka kwani amesema katika maandiko yake matakatifu kuwa yeye ni Mungu Mwenye wivu,” aliongeza kAskofu huyo.