Wizara ya afya katika kaunti ya Mombasa imewahimizwa wakaazi kuzingatia mazingira safi hasa msimu huu wa mvua ili kuepukana na maradhi mbalimbali ya kifya.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Waziri wa afya kaunti ya Mombasa Ibrahim Mohamed Abdi amesema kuwa lazima wakaazi wazingatie mazingira safi ili kuzuia kuchipuka kwa mkurupuko wa maradhi ambayo husababisha hasara kubwa kwa wananchi.

Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumatatu Abdi amesema kuwa wizara hiyo imepanga mikakati mwafaka ya kuhakikisha kuwa inatibu maji yote wakaazi wanayotumia ili kuzuia magonjwa huku akisema kuwa visa vyote Mombasa pia vitatibiwa.

Abdi amesisitiza umuhimu wa kuweka mazingira safi pamoja na kuchemsha maji kabla ya kuyatumia ili kuepukana na maradhi kama vile homanyongo, kipindupindu miongoni mwa magonjwa mengine.

“Tunawaomba wakaazi kuhakikisha kuwa wanayatibu maji yote ikiwmo ya visima kabla ya kuyatumia ili kuzuia maradhi mbalimbali ya kiafya kwani bila ya kuzingatia usafi hususan msimu huu wa mvua itakuwa hatari kubwa kwa afya ya wakaazi,” alisema Abdi.

Kauli ya waziri huyo wa afya kaunti ya Mombasa imejiri baada ya Shirika la Msalaba Mwekundi tawi la Mombasa kutangaza kuzuru mashinani na kutoa matibabu kwa wakaazi ya kutibu maji ili kuzuia kuchipuka kwa maardhi ya kiafya.