Waziri wa Ugatuzi Mwangi Kiunjuri amesema kuwa wizara hiyo itatenga fedha maalum katika bajeti yake ijayo kwa maseneta ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ya kutathmini utendakazi wa serikali za kaunti.
Akiongea katika kongamano baina ya maafisa wa wizara hiyo na Tume ya Seneti ya Ugatuzi katika kaunti ya Mombasa siku ya Jumatatu, Kiunjuri alisema kuwa itakuwa bora iwapo watashirikiana kuhakikisha kuwa ugatuzi unamfaa mwamanchi wa kawaida.
Aidha, waziri huyo alisema kuwa wizara hiyo itatoa mafunzo kwa wananchi kuhusu majukumu ya afisi ya seneta.
Alitoa wito kwa wabunge kubuni sheria ya kuwezesha maseneta kupokea fedha kutoka kwa serikali kuu.