Mwenyekiti wa shirika la utunzi wa mazingira Kanda ya Ziwa Michael Otieno, ametoa wito kwa wizara ya uvuvi kutatua changamoto zinazoiathiri sekta ya uvuvi nchini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Katika mahojiano na mwanahabari wetu jijini Kisumu mapema Jumatatu, Otieno alisema chemi chemi za maji zinaharibiwa kwa kuchafuliwa kila mara, hivyo basi kusababisha vifo vya Samaki Ziwani Victoria.

Aliongeza kuwa baadhi ya wavuvi hutumia neti zisizofaa kuvua samaki, na kusababisha kuvuliwa kwa samaki ambao hawajakomaa.

Nyaguti alisema kuwa hicho ndio chanzo, cha kupungua kwa kasi kwa samaki ziwani humo.

“Ukweli ni kwamba wizara ya uvuvi, haijafanya lolote kufikia sasa kuzuia uvuaji wa samaki wachanga,” alisema Otieno.

Vile vile, aliyataka mabunge ya kaunti zinazopakana na Ziwa Victoria kutunga sheria mwafaka za kuwawezesha wavuvi kujiimarisha kiuchumi kupitia uvuvi.

Alisema sekta hiyo imezongwa na ufisadi, akisisitiza kuhusu umuhimu wa kuwepo kwa sheria bora za kukomesha uovu huo.

“Mabunge ya kaunti zinazopakana na Ziwa Victoria, yanafaa kutunga sheria mwafaka za kuwawezesha wavuvi kujiendeleza. Wavuvi hawafai kudhulumiwa na kukandamizwa,” aliongeza mwenyekiti huyo wa Shirika hilo.