Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamme mmoja mwenye umri wa umri wa makamo, alifikishwa kwenye mahakama ya Winam jijini Kisumu mnamo Jumatatu na kushtakiwa kwa wizi wa mabavu.

Mahakama iliambiwa kuwa George Otieno alivunja makaazi ya James Orina Ogeto usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita mtaani Manyatta jijini Kisumu.

Alidaiwa kuiba viatu, shilingi alfu mbili pesa taslimu na simu ya rununu yenye thamani ya shilingi alfu mbili.

Mshtakiwa alikanusha mashtaka mbele ya hakimu Carolyne Njalali.

Aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi alfu 80, na kesi hiyo kupangiwa kusikilizwa tarehe 7 mwezi ujao.