Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae amesema zahanati iliyoko eneo la Nubia karibu na mji wa Kisii itafunguliwa hivi karibuni ili kutoa huduma za matibabu kwa wakazi wa eneo hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana na Ongwae, wengi wa wakazi hulazimika kutembea hadi hospitali ya rufaa na mafuzo mjini Kisii kutafuta matibabu na kutohudumiwa kikamilifu kufuatia msongamano wa wagonjwa, na kusema hivi karibuni zahanati hiyo itafunguliwa kwani mikakati yote imeimarishwa kufikia sasa.

Aidha, alisema zaidi ya zahanati 70 katika kaunti hiyo hazijafunguliwa, baada ya serikali ya kitaifa kugatua sekta ya afya na kuahidi kujaribu kila awezalo kuhakikisha zinafunguliwa moja baada ya nyingine ili sekta ya afya kuimarishwa zaidi.

“Zahanati ya Nubia itafunguliwa ili wakazi wale wanatembea mbali kutafuta matibabu muwe mnatibiwa karibu na zahanati hiyo,” alisema Ongwae.

“Kuna zahanati nyingi ambazo zilijengwa na serikali ya kitaifa na tulikabidhiwa zote baada ya sekta ya afya kugatuliwa, na bado zahanati hizo hazijafunguliwa lakini tutahakikisha zahanati hizo zimefunguliwa,” aliongeza Ongwae.