Zaidi ya asilimia 50 za baa jijini Naivasha zimefungwa kufuatia agizo la bodi la kuthibiti vinywaji kwa kutofikia kiwango kinachohitajika kufanya biashara.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana na msimamzi wa kata ndogo ya Naivasha Julius Nyata, baa 564 zilijipatia leseni mpya kupitia bodi mpya ya kuthibiti vinywaji.

“Baa ambazo zilikua zinafanya biashara karibu na vyumba vya kupanga na karibu na shule zote zimefungwa,” alisema Nyata. “Tutafuatilia baa 223 katika wiki zijazo ili kuhakikisha zinafanya kazi kulingana na leseni tulizowapa," aliongeza. 

Akiongea jijini Naivasha Jumamosi, Nyata alisema kwamba baa ambazo zinaendeleza biashara karibu na reli zitafungwa pia.

Baa nyingi zaidi Mai-Mahiu zimefungwa kufuatia kesi nyingi za ujambazi kuripotiwa huko.

“Ukahaba ulikua umekithiri katika baa nyingi Mai-Mahiu,” aliongezea Nyata.