Baadhi ya maeneo katika eneo bunge la Nyali yalioathirika na mafuriko. [Picha: Said Abdalla Saido/ facebook.com]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Takriban nyumba 50 zimeathirika na mafuriko katika mtaa wa Matopeni Kongowea katika eneo bunge la Nyali kufuatia mvua kubwa inayonyesha.Baadhi ya wakaazi wa eneo hilo wamelazimika kukita kambi katika nyumba za wazee wa mitaa zilizoko katika maeneo salama, baada ya nyumba na maduka yao kufurika.Wakaazi hao, wakiongozwa na Hamisi Suleimani ambaye ni mzee wa mtaa, wameitaka serikali kuu na ile ya kaunti kuingilia kati na kutoa msaada wa dharura kwao.Hata hivyo, baadhi ya vijana wamejipatia ajira kutokana na mafuriko hayo, baada ya kuanza biashara ya kuvukisha watu kutoka upande mmoja hadi mwingine.Kwa upande wake, Gavana Hassan Joho amesema kuwa serikali ya kaunti italazimika kubomoa baadhi ya kuta ambazo zinazozuia maji kupita, ili kuzuia mafuriko.Akizungumza siku ya Jumanne baada ya kutembelea familia zilizopoteza wapendwa wao baada ya kuangukiwa na ukuta, Joho alisema watafanya mazungumzo na wamiliki wa kuta hizo kabla ya kuzibomoa.Vile vile, alisema kuwa serikali yake imeanzisha mradi wa kuwapa chakula walioathirika na mafuriko hayo.