Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Zaidi ya vijana mia mbili toka eneo bunge la Bahati waliofuzu kwenye mafunzo ya uendeshaji magari walipata hati zao walipokabidhifa ofisini za CDF Bahati Jumatatu.

Wakizungumza baada ya kupewa hati muhimu, vijana hao walisema wameshukuru ofisi ya mbunge huyo Kimani Ngunjiri ambayo imewasaidia kupata hati hizo jambo ambalo walitaja kama njia mojawapo ya kumaliza umaskini na kuleta ajira miongoni mwa vijana.

"Tunashukuru mbunge wetu kwa kutupa fursa ya kupata mafunzo ya kuendesha magari bila malipo, tumefuzu na tuna imani kuwa tutaweza kupata ajira kwenye mashirika mbali mbali inje na ndani ya kaunti ya Nakuru," alisema Grace Nyawira ambaye nimsemaji wa vijana toka wadi ya Kiamaina.