Zaidi ya visima 600 vya maji vitatibiwa ifikapo mwishoni mwa zoezi la kukabiliana na ugonjwa wa hepatitis A linalo endelezwa na serikali ya kaunti ya Mombasa kwa ushirikiano na wakfu wa Shariff Nassir.
Haya yamefichuliwa na waziri wa afya kaunti ya Mombasa Mohammed Abdy.
katika kikao na wandishi wa habari siku ya Ijumaa, Abdy amesema kufikia jana jioni zaidi ya vyungu 100 vyenye dawa ya kutibu maji yaani chlorine vilichukuliwa na wananchi na kutia visimani kama hatua ya kukinga maji dhidi ya viini hivyo.
Waziri huyo amesema zoezi la kukagua maji ya chupa yanayo uzwa barabarani linaendelezwa katika maabara za kaunti na kutoa wito kwa wananchi kuwa makini na vyakula ama maji yauzwayo barabarani.
Kauli ya Abdy inajiri wakati ambapo zaidi ya watu 120 wakiwa tayari wameathirika na ugonjwa huo wa hepatitis A kaunti ya Mombasa.