Zoezi la kugawa sehemu ambapo zaidi ya wachuuzi 2,000 walioondolewa kutoka katikati mwa mji wa Nakuru na kupelekwa nyuma ya barabara ya Oginga Odinga watakapohudumia inaendelea humo.
Zoezi hilo linafanywa na viongozi wa kutoka serikali ya jimbo chini ya ulinzi mkali, na ambalo limewezesha kwa serikali hiyo kuchukua barabara mbili za umma, ambazo zinadaiwa kunyanukuliwa na watu binafsi.
Aidha, imebainika kuwa ingawa si wafanyabiashara wote waliofurushwa mjini watapata nafasi katika mahala hapo, serikali ya jimbo la Nakuru imesimama kidete kwamba wafanyabiashara wote sharti wapate mahala mbadala ambapo watafanyia kazi zao.
Hata hivyo, kwa mjibu wa mmoja wa wachuuzi hao Kahiga Karanja ameikumbatia hatua hiyo akihoji kuwa ni hatua itakayopunguza msongamano mjini huku, akihoji kuwa japo zoezi hilo litalemaza biashara zao kwa muda zitaimarika baadaye
Zoezi hilo linajiri huku upande mmoja wa wachuuzi ukiishtaki serikali ya jimbo na kesi hiyo ikitarajiwa kusikizwa jumatatu ijayo.