Zaidi ya Wanafunzi elfu 13 kutoka shule za upili, vyuo vya kadri na vile vikuu kaunti ya Mombasa wamenufaika na ufadhili wa karo kutoka kwa Serikali ya kaunti ya Mombasa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho alisema kuwa mradi huo umegharimia zaidi ya shilingi milioni 110 kuwasaidia wanafunzi hao kujiendeleza kimasomo.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumamosi, Joho alisema kuwa wanafunzi watakaoangaziwa zaidi ni wale wa shule za upili, vyuo na wenye mahitaji maalum.

“Mradi huu utaangazia zaidi wanafunzi wasiojiweza na wenye mahitaji maalum hususan wanafunzi wa shule za upili, na vyuo kama njia moja wapo ya kuinua viwango vya elimu,” alisema Joho.

Joho alidai kuwa kupitia kwa mradi huo, kaunti ya Mombasa itawawezesha wanafunzi kufanya vyema katika mitahini ya kitaifa kwani wengi hupitia changamoto.

Mradi huo utafanywa kila mwaka ili kuhakikisha kuwa maswala ya elimu kaunti ya Mombasa yanapewa kipau mbele.