Baadhi ya wakazi wa kaunti ya Nyamira wameitaja ziara ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kwenye ngome ya kisiasa ya upinzani kule Nyamira kama mbinu muungano wa Jubilee unatumia ili kuyeyusha uungwaji mkono wa muungano wa Cord katika eneo hilo. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Haya yanajiri baada ya wabunge wote wanne kutoka kaunti hiyo na wanaoegemea mrengo wa upinzani Cord, akiwemo mbunge wa Kitutu Masaba Timothy Bosire ambaye kwa muda amekuwa akiikosoa vikali serikali ya Jubilee kuonekana hadharani wakimkaribisha Rais na naibu wake. 

Ikumbukwe kuwa baadhi ya wabunge wa muungano wa Cord kutoka eneo hilo wamekuwa wakiisuta serikali ya Jubilee kwa kutelekeza eneo la Gusii kimaendeleo, na hata baadhi yao kuapa kutoandamana na Rais kwenye ziara zake Gusii kinyume na ilivyo shuhudiwa jana.