Ziwa la Nakuru ambalo ni mojawapo za mbuga za wanyama nchini inaendelea kuharibiwa na utupaji kiholela ya takataka ya plastiki. Hii ni kulingana na usimamizi wa KWS ambao imetoa wito kwa serikali ya kaunti kupiga marufuku utumizi wa vyombo vya plastiki kwenye mbuga hiyo.
Kulingana na Dickson Ritan ambaye ni mlinzi mkuu wa KWS, taka ya aina hii inahatarisha maisha ya wanyama wa majini.
“Matumizi ya plastiki ikizidi, wanyama wa majini wataangamia na pia wale wa ugani pia watakua matatani iwapo watakula hizi plastiki,” alisema bw Ritan.
Kulingana na ripoti ya takwimu iliyofanywa mwaka wa 2015, zaidi ya tani ishirini ya plastiki ilipatina kando kando ya ziwa la Nakuru.
“Serikali ya kaunti ya Nakuru inafaa kufanya haraka ili kuokoa rasilmali hii,” alisema Bw Ritan.