Zoezi la usajili la makurutu katika eneo bunge la Mvita mjini Mombasa limekubwa na changamoto pale baadhi ya makurutu walipozimia kufuatia zoezi la makurutu na kukosa huduma ya kwanza.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwakilishi wa Wadi ya mji wa Kale Murfad Abdallah alikosoa hatua hiyo akidai kuwa ni aibu kubwa na serikali ya kaunti, Shiraka la Msalaba Mwekundi na polisi wa huduma ya kwanza kukosekana na maeneo hayo ya zoezi hilo.

Abdallah amewataka wahusika kuwa waangalifu katika maeneo kama hayo ili kuzuia kushughudiwa kwa majanga kutokea.

"Tunahuzunika kuona zoezi hili likikosa watu wa kutoa huduma ya kwanza kwa jamii hasa Shirika la Msalaba Mwekundu, serikali ya kaunti ya Mombasa, na kuomba hali hii isitokee tena na wakati wa zoezi hili lazima maafisa kama hao kuhudhuria ili kuzuia majanga",alisema Abdallah wakati wa zoezi hilo mjini Mombasa siku ya Jumatatu.

Wakati uo huo, Afisa mkuu wa Polisi anayesimamia zoezi hilo na ambaye pia ni afisa mkuu wa Polisi mjini Kilifi Alexander Makau amewahimiza vijana kujitokeza kwa wingi huku akisema kuwa wakaazi wa eeno hilo ndio watapewa nafasi ya kwanza.

Photo: Zoezi la Makurutu likiendelea Mombasa, maafisa wa polisi wanasema usajili wa makurutu utapewa wakaazi wa eneo hilo kwanza.