Gavana Ali Hassan Joho amewashukuru wakaazi wa Mombasa kwa kumchagua kama kiongozi wao na kusimama naye kila anapojaribu kuyumbishwa na mahasidi wake wa kisiasa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Amewakashifu wanaotaka kumuangusha kisiasa na kusema kamwe hawataweza.

Joho alitoa mfano wa hapo awali ambapo alibandikwa jina Sultan.

Kulingana naye, alibandikwa jina sultan na mahasidi wake wa kisiasa ili ionekane kwamba amejiita hivyo yeye akiwa na nia mbaya ya kuwa na uongozi wa kiimla dhidi ya wa-Mombasa na wapwani kwa ujumla.

"Mahasidi wangu wa kisiasa waliniita majina ikiwemo Sultan ili kuharibu jina langu na kunitenga na wakenya. Waliita hata mkutano wa wanahabari wakidai kwamba nilitaka kuwa Sultan, mfalme ili kuwakandamiza," alisema Joho.

Akizungumza Jumanne wakati wa ufunguzi wa hafla ya Pili ya Uhamasishaji wa Ugatuzi (Second Devolution Sensitization Week) katika uwanja wa Makadara, Joho alisema mahasidi hao walipigwa na butwaa ilipobainika kuwa jina sultan lilipendwa sana na wakenya.

"Badala ya kunishtuma, wakenya walipendezwa sana na jina Sultan na kuwaacha maadui hao kwa mshangao. Napendwa na watu," aliongezea.

Soma: [Video]: Junet explains why Uhuru is a 'Muthamaki', and Joho 'Sultan'

Gavana huyo ambaye anataka urais mwaka wa 2022, alisema ugatuzi umeimarishi huduma mbali mbali Mombasa na kuitaka serikali kuu kutoa pesa za kutosha kwenye serikali za kaunti tena kwa wakati ufaao.

#hivisasaoriginal